♨♨♨♨♨♨♨♨♨♨
*SOMO(1): SIFA NA KUABUDU (PRAISE AND WORSHIP).*
*MAMBO SABA MUHIMU YA KUYAFAHAMU KUHUSU IBADA NA SIFA*
*1. SIFA NI MAKAO YA MUNGU* – ni mahali akaapo au aketipo Mungu.
• Makao ni kiti, nyumba(hekalu), mji; mahali pa kuishi – patakatifu pake aliye juu (palipoinuka).
• Mungu huketi katika Sifa za Israeli – Zaburi 22:3.
• Hivyo ni lazima uyaheshimu makao ya Mungu.
• Usiyanajisi makao ya Mungu.
• Usijiinue, usiwe na kiburi, uwe mnyenyekevu mbele za Mungu na wanadamu.
• Sifa ni hekalu la Mungu – ni lazima kusifu kuwe safi na kwa utakatifu.
• Unaposifu ujazo wa Roho Mtakatifu huja; yaani Mungu huja kukaa katika makao yake.
• Uunapomsifu Mungu unaenda kwenye makao ya Mungu moja
kwa moja.
• Shetani alitaka kuyapindua makao ya Mungu mbinguni, na hata makao ya Mungu kupitia sifa! Anataka asifiwe
yeye badala ya Mungu; lakini Mungu ameahidi kuyarejesha mambo yote kuwa mapya!
• Mungu anaheshimu sana sifa na kuabudu, hata amesema sifa zake hatazipa sanamu!
*2. SIFA NI MADHABAHU YA KUTOLEA SADAKA MBELE ZA MUNGU ALIYE HAI.*
• Madhabahu ni meza au mahali pa kutolea sadaka mbele za Mungu – dhabihu ya sifa.
• Hivyo: usimchanganye kwa kuishiriki meza ya BWANA YESU na meza ya mashetani (1Kor.10:20-22).
• Usiimbe nyimbo zisizo maana za kiduniani au za kishetani!
• Usilete mitindo ya duniani mbele zake Mungu.
• Ukiona madhabahu unapata mvuto wa uwepo wake Mungu na kuabudu – sifa hukuvutia kuabudu.
• Ujitakase na umtakase Mungu uikaribiapo madhabahu ya Mungu- yaani sifa. (Walawi 10:3)
*3. SIFA NI SADAKA / DHABIHU YA KUMTOLEA MUNGU.*
• Usichanganye sehemu ya kuitolea (Zaburi 126:1-2)
• Usilete sadaka / uvumba wa kigeni (manukato) ya kigeni.
• Sifa na kuabudu ni manukato / harufu nzuri mbele za Mungu.
• Badala ya sisi kutoa wanyama kuwa harufu ya kupendeza mbele za Mungu, sisi tunatakiwa kutoa dhabihu ya sifa. (Waebrania 13:15)
• Ni dhabihu ya kuitoa miili yetu – ni dhabihu hai iliyo takatifu mbele za Mungu. (Zaburi 40:6)
• Shetani / ibilisi alikuwa ni kwayamasta (Lusiferi = nyota ya asubuhi (kupendeza, kiongozi); nyota = malaika, Ayubu 38:7) (Ezekieli 28:13;) ambaye alitakiwa kuitumia karama hii kwa ajili ya utukufu wa Mungu; lakini akaitumia vibaya, badala ya kumtukuza Mungu na kumtolea dhabihu ya sifa Mungu, akajitolea yeye mwenyewe na akawataka na wengine wote wamsifu yeye badala ya Mungu.
• Leo hii, wengine wanajisahau vivyo hivyo, waimbaji maarufu wamejisahau: badala ya kumtolea Mungu dhabihu ya sifa na kuabudu, wanajitolea wao wenyewe, wanawataka watu wawatolee wao sifa au wanamtolea shetani badala ya Mungu anayestahili sifa na utukufu wote!
• Kama kiongozi wa sifa na kuabudu au uimbaji ongoza sifa vizuri, kwani ni hatari kuzitwaa sifa za Mungu na kumpa mwingine au kujipa sifa wewe mwenyewe.
• Hebu fikiria, unapoimba na kucheza miziki ya disco, dansi, na uimbaji mwingine usio wa kumsifu Mungu, unamtolea sifa nani? Kama sio wewe mwenyewe, mtu mwingine au shetani?
• Hebu soma kitabu cha nabii (Isaya 42:8).
*4. KUSIFU NA KUABUDU NI SILAHA YA VITA VYA KIROHO.* (Zaburi 149:6-3)
• Iliyotumika kuangusha ngome na kuta za Mji wa Yeriko.
• Ilitumiwa na Yehoshafati kuwashinda maadui.
• Iliyotumiwa na Paulo na Sila kuwafungua vifungo na kufungua milango ya gereza.
• Ni silaha inayoangusha ngome za shetani, wachawi, na kazi za shetani (Fikira, mawazo, na kila kijiinuacho juu ya elimu ya Mungu).
• Tusiache kuitumia silaha hii na wala tusimuachie shetani aitumie na kutuangamiza sisi badala yake.
• Ni njia ya kumfunga yule mwenye nguvu (shetani, ibilisi na majeshi yake yote) – Zaburi 149:7-8
• Ni silaha ya kuleta uamsho wa kiroho kwa mwamini mwimbaji na kwa kanisa.
• Sifa huleta upako na utukufu wa Mungu kwa muimbaji na kwa kanisa, wenye kuziharibu na kuzibomoa kazi za shetani.
*5. KUSIFU NA KUABUDU NI HUDUMA YA KIROHO NA NI CHOMBO CHA HUDUMA YA KIROHO.*
• Ni chombo cha huduma ya mawasiliano na Mungu.
• Kuruhusu utendaji wa karama na huduma za Roho Mtakatifu.
• Ni chombo cha kusemezana (kusema zamu kwa zamu, mmoja anazungumza na mwingine anajibu; kuhojiana) na Mungu.
• Ni chombo cha huduma ya neno la Mungu kwa njia ya kuonya, kufundisha, kuelekeza, kuhubiria injili, kuwatia moyo watu wa Mungu, kukemea na kufariji, na kumbariki Mungu.
• Ni chombo cha kulijenga kanisa la Mungu.
• Ni chombo cha utumishi ambacho kila mtu anatakiwa akitumie ili kumtumikia Mungu – kila mwenye pumzi!
• Ni amri ambayo kila mwenye pumzi anatakiwa akitumie chombo hiki na pia atakitolea hesabu kwa Mungu (atawajibika) kuhusu matumizi yake.
• Ni chombo cha huduma ya utumishi kwa Mungu, kanisa, na kwa ulimwengu.
• Ni huduma ya utumishi wa milele mbele za Mungu sasa na hata kule mbinguni wanadamu pamoja na malaika watakatifu wa Mungu.
*6. KUSIFU NA KUABUDU NI CHOMBO AU NJIA YA UTAKASO.* (Mithali 27:20)
• Kusemezana humtakasa mtu – Isaya 1:18; Mathayo 17:1-3
• Unapokuwa mtu wa kupenda kusifu na kuabudu, mawazo mabaya huondoka akilini, hisia, nia na dhamiri
mbaya huondoka; kisha moyo hujaa Neno la Mungu.
• Uimbaji katika Roho na kweli hujenga kiroho; mwimbaji, kanisa, na ulimwengu.
• Ni chombo ambacho humfanya mtu kung’aa na kupendeza mbele za Mungu na hata mbele za wanadamu; sababu ya kufunikwa na utukufu wa uwepo na upako wa Mungu.
• Kusifu na kuabudu ni pambo zuri la kiroho; Mungu huwapamba wateule wake kupitia sifa na kuabudu (Zaburi 149:1-5)
*7. SIFA NA KUABUDU NI CHOMBO AU MFUMO WA KUTENGENEZEA BARAKA ZA MUNGU.*
• Ni kama mzunguko wa maji kutoka mvuke, kuwa mawingu, kuyeyuka na kuwa mvua kwa joto la jua, maji
kumwagikia ardhini na kuwa sababisho la uotaji wa vyakula vingi na lishe kwa wanadamu na wanyama.
(Amosi 5:8; 9:6; Zaburi 147:7-8)
♨♨♨♨♨♨♨♨♨♨ Somo Iitaendelea
*SOMO(2): KUSIFU NA KUABUDU.*
♨♨♨♨♨♨♨♨♨♨
NI MUHIMU SANA! MAENEO MAKUU MATATU YA MSINGI KUYAFAHAMU KUHUSU SIFA NA KUABUDU ILI UWEZE KUSIFU NA KUMUABUDU MUNGU KATIKA ROHO NA KWELI.
*1). KUMSIFU MUNGU (SIFA, PRAISE).*
*• Ni kuonyesha hali ya kumkubali na kumfurahia Mungu kwa matendo yake, bila kujali kama umefaidika au la!*
• Ni kutengeneza mazingira na kuonyesha kwake Mungu mwenyewe, na kwa wengine; kwamba anakubalika kwa
uzuri na kwa kupendeza kwa matendo yake ayatendayo na hata vile Mungu mwenyewe alivyo, au hali ya kumfurahisha Mungu kwa yale yote aliyotenda, anayoyatenda, na atakayoyatenda; kwake Mungu mwenyewe, kwako, na kwa wengine wote.
• Hivyo basi kusifu kunahusu kuonyesha kufurahia, kumfurahia na kumfurahisha Mungu.
*2). KUMUINUA MUNGU ( ADORATION = To adore God)*
*• Ni kiini au moyo wa kumsifu, kumuabudu, na kumuomba Mungu.*
*• Ni eneo muhimu sana ili uwe na nguvu katika kusifu, kuabudu, na kuomba.*
*• Maana ya kumuinua Mungu ni kuwa na ile hali ya ndani ya moyoni mwako ya uelewa wa uthamani na ukamilifu wa tabia na uzuri wa Mungu katika sifa za Mungu; jinsi alivyokuwa, alivyo hivi sasa, na atakavyokuwa milele; bila kujali kuwa umefaidika chochote au la!*
• Ni kuzifurahia, kuzikubali, na kuzipenda sifa na tabia za Mungu jinsi alivyo, na kisha kumueleza yeye
mwenyewe Mungu mbele zake (si mtu mwingine) jinsi unavyomjua au unavyomfahamu kwa uzuri wa sifa na
tabia zake.
• Katika eneo hili ni lazima uzifahamu sifa za Mungu na ndipo utaweza kumuinua Mungu vizuri.
*MFANO WA JINSI YA KUMUINUA MUNGU KWA BAADHI YA SIFA NA TABIA ZA MUNGU.*
*a) Sura au umbile lako Mungu:*
• Wewe Mungu ni Roho tena Mtakatifu wa watakatifu; ni wa milele uliyekuwako, uliyeko, na utakayekuja.
• Wewe ni Mkuu sana, huna mipaka wala kizuizi.
• Uzima wako ni wa milele na milele yote.
*b) Uweza wako Mungu ni wa ajabu ya kutisha.*
• Una uweza wa milele na milele.
• Unaweza yote, wala hauchoki!
• Unajua yote, hekima na maarifa yako havichunguziki.
• Uko popote, mahali pote kwa wakati wote – hulali wala husinzii !
• Uwepo wako huleta utukufu, umeijaza mbingu na nchi, tena unapendeza na kutisha kama nini!
• Unamiliki vyote, dunia na vyote viijazavyo, pamoja na mbingu na majeshi yako yote, vyote ni vyako!
*c) Tabia zako Mungu na mwenendo wako pia havichunguziki!*
Na wala hakuna lugha itoshayo kuelezea uzuri wake!
• Maana msimamo wako ni wa milele katika utakatifu wa utakatifu wote!
• Wewe Mungu unatenda mema, kwako hakuna tendo lolote baya kamwe!
• Huna kigeugeu wala kivuli cha kugeuka geuka – haubadiliki kamwe msimamo wako!
• Umejaa huruma, rehema, na fadhili za milele na upendo wa milele!
• Ni Mungu mwenye utukufu mwingi.
*d) Mapenzi yako ni mema!*
• Wewe Mungu unapenda mema na unachukia dhambi na ubaya wote!
• Ni Mungu unayetuwazia mema siku zote, maneno yako na matendo yako kwetu ni kwa mapenzi yako mema – nasi katika hayo yote tunauona uzuri wako mkuu ajabu!
• Unayakubali mema na kuyakataa mabaya yote!
• Unachukia mabaya na dhambi za waovu, bali unawapenda viumbe wako wote, wema na wabaya!
• Kwa neno lako umetujulisha mapenzi yako kwamba-hakuna atakayetutenga na upendo wako Mungu!
*e) Jina lako:*
• ni kuu, takatifu sana, na tukufu sana.
• Linauweza na nguvu za milele.
• Lina mamlaka yote.
• Ni ngome na thawabu kubwa sana kwa kila akuaminiye – kwa uponyaji, ulinzi, msaada, na wokovu; tena ni silaha bora sana!
*f) Njia zako:* ( kawaida, desturi, kanuni, taratibu, siri, amri, na mapito yako yote)
• Hazichunguziki, hazitafutikani, hazifananishwi!
• Ni za hekima na maarifa makuu sana kupita wote!
• Wewe ni Mungu wa maagano na kweli.
*g) Neno lako:*
• Ni la milele, halina makosa, hata hivyo tazama; umelihakikisha tena mara saba!
• ni uzima, ni nuru, ni taa na mwangaza kwetu,
• ni kali kuliko upanga uwao wote ukatao kuwili.
*h) Kazi zako na huduma zako kwa wote.*
• Ni kuu na za ishara maajabu na miujiza mikuu.
• Unaokoa na kukomboa – wewe ni shujaa wa wema wote!
• Uumbaji wako ni mkuu wapendeza sana.
• Unatoa Karama na huduma zako kwa wanadamu tuwe mawakili tu!
• Unazivunja na kuziharibu kazi zote za shetani ili kututetea na kutuponya wanadamu tusionewe na kuharibiwa na shetani – tena na tazama, umetupa amri na uwezo wa kukanyaga nyoka na nge na nguvu zote za yule mwovu, wala hakuna kitakacho tudhuru!
• Kazi zako zinapendeza, unazozitenda ndani ya watu kupitia watu wote na hasa wale walioitwa kwa jina lako!
• Wewe ni Mungu uletaye neema, kweli na uzima wa milele kupitia mwanao na BWANA WETU YESU KRISTO.
*i) Wastahili wewe BWANA:*
• Kujulikana mbinguni na duniani kote kuwa ndiwe Mungu pekee!
• Utukufu wote, heshima zote, adhama, ukuu, enzi na mamlaka yote!
• Kusifiwa, kuinuliwa, kuabudiwa na kutukuzwa milele kuliko wote na kupita miungu yote.
• Kumiliki, kutamalaki, kutawala vyote milele!
*MATOKEO YA KUMUINUA MUNGU.*
• Utapata amani moyoni ya kumwendea Mungu (Ayubu 22:21)
• Utayaona mambo mengine yote kuwa ni hasara (kama mavi) bali Mungu peke yake kuwa ni wa thamani kubwa
sana kwako na kwa wote! (Wafilipi 3:8)
• Utakua na kuongezeka imani ambavyo ndiyo msingi wa kusifu, kuabudu na maombi safi mbele za Mungu (Ebr.11:6)
• Utapata ujasiri yaani - hutakuwa na hofu ya ghafla, woga, mashaka, na wasiwasi.
• Utakuwa na utayari kwa lolote lile kwa ajili ya Mungu, hata kufa kwa ajili yake!
*3). KUMUABUDU MUNGU (KUABUDU = WORSHIP)*
• Ni udhihirisho moyoni na kwa nje hali ya uelewa wa ndani moyoni kuhusu uthamani wa Mungu alivyokuwa,
alivyo sasa, na atakavyokuwa milele.
• Ni kuidhihirisha kwa nje ile hali ya kumuinua Mungu kwa njia ya maneno na kwa kuonyesha vitendo katika mwili; kama vile, kuimba, kupiga magoti, kuinua mikono, kulala kifulifuli, kutoa sadaka, kusaidia masikini, kuhubiri neno, kusikiliza na kujifunza neno la Mungu, kuhudhuria ibada n.k.
• Ni udhihirisho kwa vitendo jinsi unavyomtambua, unavyomthamini, unavyomjali, unavyompenda, unavyomheshimu, unavyomwona Mungu wako kuwa ni wa thamani kuu sana na ngao na thawabu kubwa sana kwako!
• Ili kuweza kumuabudu Mungu vizuri, ni lazima uive kwanza katika hali ya kumuinua Mungu ndipo utaweza
kumuabudu Mungu vizuri sana katika Roho na kweli!
• Ni kumueleza Mungu na kumwonyesha kwa vitendo mbele zake, jinsi sasa unavyojisikia vizuri sana kwa kuwa pamoja naye na mbele zake maishani mwako!
• Ndiyo maana mtu aliyeiva vizuri sana katika kumuabudu Mungu, yupo tayari kufanya chochote kwa ajili ya Mungu yule anayemwamini na kumuabudu!
• Watu wengi leo hudai wanamuabudu Mungu, lakini kumbe bado hawapo katika hali ya kumuinua, ndiyo maana hushindwa kumuabudu Mungu ipasavyo na ibada zetu zinakuwa kavu tu.

Maoni
Chapisha Maoni