VIKOA VYA MAANA Dirk (2010), anasema kuwa vikoa vya maana ni jozi za maneno yenye maana zinazohusiana ambazo maana zake zinategemeana na kwa pamoja zinatoa dhana ya kimuundo yenye uhalisia ndani yake . Hii humaanisha kwamba, maana ya haiponimu zinazotokana na kikoa kimoja hujumuishwa katika maana pana au jumuishi moja. Wikipedia , wanaeleza kuwa kikoa cha maana ni msamiati wa kiufundi katika taaluma ya isimu ambao unaeleza kikundi cha maneno yanayohusiana kimaana. Mahusiano ya maana katika vikoa vya maana huwa na sifa kuu mbili: · kila kikoa kinaweza kuzaa vikoa vingine vidogo vidogo. Kwa mfano; Matunda . 1. Maembe, 2. Machungwa, na 3. Papai. · Hakuna kanuni ya upangaji wa hivyo vikoa. Kwa mfano; Matunda 1. Papai 2. ...