Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

VIKOA VYA MAANA

VIKOA VYA MAANA Dirk (2010), anasema kuwa vikoa vya maana ni jozi za maneno yenye maana zinazohusiana  ambazo maana zake zinategemeana na kwa pamoja zinatoa dhana ya kimuundo yenye uhalisia ndani yake . Hii humaanisha kwamba, maana ya haiponimu zinazotokana na kikoa kimoja hujumuishwa katika maana pana au jumuishi moja. Wikipedia , wanaeleza kuwa kikoa cha maana ni msamiati wa kiufundi katika taaluma ya isimu ambao unaeleza kikundi cha maneno yanayohusiana kimaana. Mahusiano ya maana katika vikoa vya maana huwa na sifa kuu mbili: ·          kila kikoa kinaweza kuzaa vikoa vingine vidogo vidogo. Kwa mfano; Matunda . 1.       Maembe, 2.       Machungwa, na 3.       Papai. ·          Hakuna kanuni ya upangaji wa hivyo vikoa. Kwa mfano; Matunda 1.       Papai 2.    ...

USHAIRI

USHAIRI Kuna mitazamo ya aina mbili katika kuelezea dhana ya ushairi. kuna wanamapokeo na mamboleo. Hata hivyo kabla ya kuendelea zaidi kuwachambua tuangalie wataalam mbalimbali wanavyofasili dhana hii . Dhana ya ushairi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake. Baadhi ya wataalam hao ni kama ifuatavyo: MAPOKEO   Mssamba, (2003) akimnukuu Shaban Robert, anasema; “ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa na sanaa ya vina ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.” Mnyampala (1970) anasema kuwa “ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho kitu kilichobora sana maongozo ya Dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalum.” Amri Abeid (1954:1) anasema kuwa “ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana.” Abdulatifu  anasema kwamba ushairi ni ule ulio na sifa ya ulinganifu wa vin...

UCHAMBUZI WA RIWAYA ZA “NAGONA” NA “MZINGILE”

UCHAMBUZI WA RIWAYA ZA “NAGONA” NA “MZINGILE” 1.0 Utangulizi Katika makala haya tutachambua riwaya za ‘Nagona’ na ‘Mzingile’. Katika kuchambua riwaya hizi tutajikita katika kuangalia baadhi ya vipengele kama dhamira, falsafa, lugha, mtindo wa usimulizi, wahusika, motifu na suala la ontolojia. 2.0 Maelezo kuhusu mwandishi na riwaya zake 2.1 Maelezo kuhusu mwandishi Euphrase Kezilahabi alizaliwa mwaka 1944 katika kijiji cha Namagondo kilichoko kisiwani Ukerewe katika ziwa Victoria nchini Tanzania. Alipata elimu ya msingi huko kijijini Ukerewe na baadaye alijiunga na seminari ndogo ya Nyegezi kwa ajili ya masomo ya upili. Baada ya kumaliza alijiunga na Chuo Kikuu cha Dar es salaam mnamo mwaka 1967. Katika masomo yake alijishughulisha na nadharia mbalimbali zihusuzo falsafa (Wamitila 1991:64). Mnamo mwaka 1976 alitunukiwa shahada ya umahiri ya Chuo Kikuu cha Dar es salaam, kabla ya kutunukiwa shahada nyingine ya umahiri ya Chuo Kikuu cha Wisconsin-Madison mwaka 1982. Mwaka...