Ruka hadi kwenye maudhui makuu

Machapisho

Inaonyesha machapisho kuanzia 2017

HISTORIA YA MUHAMMED SAID ABDULLA, SAID AHMED MOHAMED NA EUPHRASE KEZILAHABI

MUHAMMED SAID ABDULLA  Muhammed Said Abdulla alizaliwa April 25, 1918, Makunduchi, Zanzibar katika familia ya kiisramu. Alipata elimu yake ya sekondari katika shule ya wamisionari (missionary school) na baada ya kuhitimu mwaka 1938 alianza kufanya kazi ya ukaguzi (Inspector) katika idara ya afya (civil health depertment). Baada ya miaka 10 aliamua kuwa mwandishi wa habari, na mhongo mmoja baadae alikuwa mhariri msaidizi wa Al Falaq, Al Mahda, na Afrika Kwetu. Mwaka 1958 alikuwa mhariri wa gazeti lililoitwa mkulima (the national agricultural magazine) ambapo hadi kustaafu kwake alikuwa akifanya kazi ya uhariri wa gazeti hilo mwaka 1968. Baada ya Abdulla kuwa mhariri katika gazeti la mkulima ndipo mafanikio yake ya mwanzo katika uandishi wa riwaya yalipoonekana baada ya kuandika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale (“1960 “Shrine of the Ancestors”) na ndiyo kazi nzuri ya Kiswahili ya mwanzo ambayo iliingizwa katika mashindano ya mwaka 1957-58 yaliyofanya na taasisi ya Fasihi ya Af...

VIKOA VYA MAANA

VIKOA VYA MAANA Dirk (2010), anasema kuwa vikoa vya maana ni jozi za maneno yenye maana zinazohusiana  ambazo maana zake zinategemeana na kwa pamoja zinatoa dhana ya kimuundo yenye uhalisia ndani yake . Hii humaanisha kwamba, maana ya haiponimu zinazotokana na kikoa kimoja hujumuishwa katika maana pana au jumuishi moja. Wikipedia , wanaeleza kuwa kikoa cha maana ni msamiati wa kiufundi katika taaluma ya isimu ambao unaeleza kikundi cha maneno yanayohusiana kimaana. Mahusiano ya maana katika vikoa vya maana huwa na sifa kuu mbili: ·          kila kikoa kinaweza kuzaa vikoa vingine vidogo vidogo. Kwa mfano; Matunda . 1.       Maembe, 2.       Machungwa, na 3.       Papai. ·          Hakuna kanuni ya upangaji wa hivyo vikoa. Kwa mfano; Matunda 1.       Papai 2.    ...

USHAIRI

USHAIRI Kuna mitazamo ya aina mbili katika kuelezea dhana ya ushairi. kuna wanamapokeo na mamboleo. Hata hivyo kabla ya kuendelea zaidi kuwachambua tuangalie wataalam mbalimbali wanavyofasili dhana hii . Dhana ya ushairi imejadiliwa na wataalamu mbalimbali huku kila mmoja akitoa fasili yake. Baadhi ya wataalam hao ni kama ifuatavyo: MAPOKEO   Mssamba, (2003) akimnukuu Shaban Robert, anasema; “ushairi ni sanaa ya vina inayopambanuliwa kama nyimbo, mashairi na tenzi zaidi ya kuwa na sanaa ya vina ushairi unaufasaha wa maneno machache au muhtasari.” Mnyampala (1970) anasema kuwa “ushairi ni msingi wa maneno ya hekima tangu kale ndicho kitu kilichobora sana maongozo ya Dunia kwa kutumia maneno ya mkato na lugha nzito yenye kunata iliyopangwa kwa urari wa mizani na vina maalum.” Amri Abeid (1954:1) anasema kuwa “ushairi au utenzi ni wimbo, hivyo kama shairi haliimbiki halina maana.” Abdulatifu  anasema kwamba ushairi ni ule ulio na sifa ya ulinganifu wa vin...