UCHAMBUZI WA RIWAYA YA WALENISI JINA LA KITABU: WALENISI MWANDISHI: KATAMA MKANGI MWAKA: 1995 MCHAPISHAJI: East African Educational Publishers Ltd. HISTORIA YA MWANDISHI Katama Mkangi ni profesa wa taaluma ya elimu-jamii. Hata hivyo ni msomi ambaye amebobea katika Nyanja mbalimbali zikiwemo lugha na fasihi ya Kiswahili. Mkangi ni mwalimu, mhadhiri na msomi ambaye amejishughulisha na masuala ya kijamii, kiuchumi, kisiasa na kiutawala; sio tu katika maandishi bali katika harakati zake za maisha ya kila siku. Itakumbukwa kuwa katika uchaguzi mkuu wa mwaka ...