MUHAMMED SAID ABDULLA Muhammed Said Abdulla alizaliwa April 25, 1918, Makunduchi, Zanzibar katika familia ya kiisramu. Alipata elimu yake ya sekondari katika shule ya wamisionari (missionary school) na baada ya kuhitimu mwaka 1938 alianza kufanya kazi ya ukaguzi (Inspector) katika idara ya afya (civil health depertment). Baada ya miaka 10 aliamua kuwa mwandishi wa habari, na mhongo mmoja baadae alikuwa mhariri msaidizi wa Al Falaq, Al Mahda, na Afrika Kwetu. Mwaka 1958 alikuwa mhariri wa gazeti lililoitwa mkulima (the national agricultural magazine) ambapo hadi kustaafu kwake alikuwa akifanya kazi ya uhariri wa gazeti hilo mwaka 1968. Baada ya Abdulla kuwa mhariri katika gazeti la mkulima ndipo mafanikio yake ya mwanzo katika uandishi wa riwaya yalipoonekana baada ya kuandika riwaya ya Mzimu wa Watu wa Kale (“1960 “Shrine of the Ancestors”) na ndiyo kazi nzuri ya Kiswahili ya mwanzo ambayo iliingizwa katika mashindano ya mwaka 1957-58 yaliyofanya na taasisi ya Fasihi ya Af...